Wafula Chebukati atoa taarifa nzito saa chache baada ya kamishna wa IEBC kujiuzulu ghafla, atoa onyo

- Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati ameelezea hofu yake kuhusu uchaguzi ujao wa Oktoba 26 - Alishiria kuwa miswada yake imepingwa na idadi kubwa ya makamishna katika tume ya uchaguzi

- Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati ameelezea hofu yake kuhusu uchaguzi ujao wa Oktoba 26

- Alishiria kuwa miswada yake imepingwa na idadi kubwa ya makamishna katika tume ya uchaguzi

- Mwenyekiti wa IEBC aliwaagiza maafisa ambao wametajwa kihasi kuhusu kuingilia uchaguzi wa Agosti 8 uliobatilishwa wajiuzulu

- Matamshi ya Chebukati yamejiri saa chache baada ya hatua ya ghafla ya ghafla ya kujiuzulu kwa kamishna wa IEBC Roselyn Akombe

- Alisisitiza madai ya Akombe kwamba ameshikwa mateka, akifichua kwamba makamishna wana ubaguzi

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Wafula Chebukati ametoa onyo kali kwa wanasiasa na maafisa wa IEBC wakati ambapo mmoja wa makamishna amejiuzulu.

Pakua APP mpya ya TUKO upate habari BURE!

Chebukati pia alisimulia kutamaushwa kwake katika kuendesha tume hiyo na kuandaa uchaguzi wa marudio uliopangiwa kufanyika Oktoba 26.

Alitoa hotuba yake Jumatano, Oktoba 18, io hiyo kamishna wa IEBC Roselyn Akombe alipojiuzulu.

Habari Nyingine: Hii ndiyo sababu ya kushtusha inayomfanya pasta maarufu kuwataka Wakenya kusimama na Uhuru kwa maombi

Habari Nyingine: Jaji Mkuu Maraga anaongea lugha ya Raila-William Ruto

Mwenyekiti wa IEBC vilevile aliwapa makataa maafisa wakuu wa tume waliotajwa kihasi na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuhusu kuingilia uchaguzi uliobatilishwa wa Agosti 8.

Raila amedai kwamba mkurugenzi wa tume hiyo Ezra Chiloba na wengine 11 ni sharti waondoke afisini ikiwa uchaguzi wowote utafanyika.

“Sitaandikisha historia kama afisa wa uchaguzi aliyesambaratisha taifa hili … sitaruhusu yeyote kuharibu taifa hili,” alisema katika taarifa nzito ambayo ilikuwa onyo fiche kwamba atajiuzulu ikiwa hali iliyopo kisiasa itaendelea.

Alifichua kwamba amekabiliwa na changamoto katika uongozi wa tume akiongeza kwamba maamuzi yake mengi ‘yamedunishwa’na makamishna wenzake.

Habari Nyingine: Babu Owino na Jaguar watwangana makonde Bungeni, yawalazimu wabunge wengine kuwatenganisha (video)

"Ni vigumu kuendesha uchaguzi wa huru na haki. Miswada yangu imeshindwa na idadi kubwa ya makamishna,” alisema.

Chebukati alisema taifa lilikuwa katika hali hatari kisiasa ambayo imezoroteshwa na kiburi cha NASA na Jubilee.

Hata hivyo alisema hatajiuzulu jinsi ilivyotarajiwa na wengi akisema ‘anaiweka Kenya mbele.’

“Tunakabiliwa na mtanziko kama taifa kutokana na hali ya kisiasa. Wakenya wana matarajio makuu kwangu lakini siwezi kuendelea na tume iliyogawanyika. Kujiuzulu kutakuwa kitu rahisi cha kufanya lakini sitafanya hivyo naiweka Kenya mbele…Nawaonya wanasiasa wanaowatishia maafisa wangu, nawapa ilani, sitaruhusu hilo,” alisema.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe?Tuma ujumbe kwa mhariri:mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaoJxhZJmrpqepaGubq%2FHnpmuo5Gptm6t06iYZqyRlr%2BqssBmpbOhpKR6tK3AZpqhmZOdsm6uwJqbmmWplnqsrcyiqqGmkWLEonnInpmcZZuqt2%2B006aj

 Share!