- Aliyekuwa mgombezi wa Urais amefunguka kuuhusu uhusiano wake na kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa, Aden Duale
- Umar alilazimika kufunguka baada ya gazeti la The Nairobian kutoa makala kuhusu uhusiano wake na Aden Duale
- Katika chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii, Umar alithibitisha kwamba walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Duale kwa muda wa miaka 3 lakini akizidi kueleza kwamba chapisho la gazeti hilo lilitia chumvi suala hilo
Pakua APP mpya ya TUKO upate habari BURE!
Gazeti la The Nairobian lilichapisha makala yaliyooshesha kwamba Aden Duale, kiongozi wa waliowengi katika bunge la kitaifa alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Nazlin Umar suala lililomfanya Umar kuvunja kimya chake.
Katika makala hayo , alinukuliwa akiomba Duale kumnunulia gari aina ya Lexus pamoja na nyumba ya kifahari.
Habari Nyingine:Mbunge wa Jubilee ataka Raila anyang'anywe paspoti kabla ya marudio ya uchaguzi
Aidha, alinukuliwa akimwita Duale kwa majina ya kimapenzi kama vile, honey, baby na majina mengine sawa.
Katika kujitetea, Umar alisema kwamba makala hayo yalitiwa chumvi.
‘Sina aibu, kuna nini mbaya na mapenzi? Ni uchungu wa mapenzi ambayo yanaumiza..katika jela ya kukimya nasalia na mshangao,’’Nazlin Aliandika.
Habari Nyingine:Hatua hii huenda ikazika NASA na vyama vingine vya Raila katika kaburi la sahau
Uhusiano wao unaonekana kukumbwa na changamoto kulingana na usemi wa Umar.
‘’NDIYO uhusiano wetu una shida na hayo mapenzi yanayolezwa kwayo hayapo.Makovu yangu hayashugulikiwi’’ Umar aliongezea.
Alieleza kwamba hakumuomba Duale Ksh 200 milioni kama ilivyoripotiwa.
Umar ameahidi kiliwasilisha kesi hiyo kortini kwa kuongezea chumvi habari kumhusu
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe?Tuma ujumbe kwa mhariri:mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaoN6fJVmpZqynJ67brvMmqlmmZaqu6jByppkpK2lncK0wYyun66rmZa7sHnWmqKeZaeWeqy1zJqnnqaqnnqvrYyam56mXZnCorjEZ5%2BtpZw%3D