-DJ na mtangazaji wa runinga Pierra Makena amemtaka Mishi Dora kumwomba msamaha kwa kumwandikia na kwa kuzungumza
-Mama huyo wa mtoto mmoja alitishia kumshtaki Mishi ikiwa hatatimiza masharti hayo katika muda wa siku saba
-Mwigizaji huyo wa Nairobi Diaries alimshambulia DJ huyo baada ya mtu aliyejifananisha na Pierra kumshambulia katika ujumbe wa Whatsapp
Mwigizaji wa Nairobi Diaries na sosholaiti mbishi Mishi Dora amepewa siku saba na DJ Pierra Makena kuomba msamaha au afikishwe mahakamani.
Habari Nyingine: Mwanamke aliyedaiwa kulala na Raila Odinga aeleza bayana kilichtokea
Mawakili wake walisema walikuwa tayari kumchukulia hatua za kisheria ikiwa Mishi hataomba msamaha kwa kuandika katika muda wa siku 7.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
DJ Pierra awali alielezea kuwa alikuwa tayari kumshtaki binti huyo kwa kumharibia jina. TUKO.co.ke inaelewa kuwa Mishi anafaa kuomba msamaha hadharani vile alimtusi DJ huyo.
Habari Nyingine: Muimbaji Jose Chameleon aoyesha mashabiki gari lake jipya la KSh24 milioni
Mwigizaji huyo tayari ameomba msamaha katika mtandao wa Instagram. Katika ujumbe mrefu, alieleza kuwa yeye alikuwa binadamu na alikuwa na uwezo wa kufanya makosa. Lakini sio wazi ikiwa tayari wameongea na kuomba msamaha kwa kinywa.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4F5hJhmm6NloJ6ys77AZqSao5Wjrm6tzK2YpJldqLy0tM6lmKKsmWK6qr%2FHomSdp6KWeqzBzqaZmmWdqK6urceaZKSZpJ64onnMrpuaZaeWerS1yq5kcGWclnq0tdWypmegpKK5