Jamaa amtaka mganga amrudishie Ksh 700,000 zake baada ya dili kuteguka

-Jamaa mmoja aliyechukua mkopo na kumlipa mganga ili amsadia kusulisha matatizo ya ndoa amesalia kwa majuto huku akimtaka mganga huyo kumrudishia hela zake -Mwanamme huyo alimpa mganga Ksh 700,000 ili mkewe apate kumrudia

-Jamaa mmoja aliyechukua mkopo na kumlipa mganga ili amsadia kusulisha matatizo ya ndoa amesalia kwa majuto huku akimtaka mganga huyo kumrudishia hela zake

-Mwanamme huyo alimpa mganga Ksh 700,000 ili mkewe apate kumrudia

Majuto ni mjukuu huja baadaye. Mwanamme mmoja kutoka kijiji cha Makuyu, eneo bunge la Maragua, kaunti ya Murang’a amebaki kwa majuto makuu baada dili kati yake na mganga kuambulia patupu.

Kwa mujibu wa gazeti ya Taia Leo, jamaa aliyetambulika kama Gathukia Kaana alikopa Ksh 700,000 na kumlipa mganga huyo ili amsaidie kumrudisha mkewe ambaye aliamua kumtoroka.

Habari nyingine:Picha 5 za sosholaiti maarufu Sanchoka zinazowapa wanaume jinamizi

Gathukia ameeleza kuwa alichukua hatua hiyo baada ya kuenda kwa wakweze mara kadhaa kwa patanisho na mkewe Nancy Muthoni bila mafanikio.

Alieleza kuwa mapenzi yake makuu kwa wanawe watano ulimpa msukumo wa mkumtafuta mkewe kwa njia zote.

‘’Baada ya kufukuzwa mara kadhaa na wakwe zangu licha ya kulipa mahari, mke wangu aliponiacha niliamua kutafuta msaada wa mganga’’ Bw.Kaana alisema kama alivyonukuliwa na gazeti la Taifa leo.

Habari nyingine:Mwanamke atoboa siri ya mumewe hadharani na kuwashangaza wengi

Alieleza kuwa mganga huyo alimuitisha Ksh 50,000 na baada ya kumpa, alumuahidi kuwa mkewe angemrudia baada ya muda wa miezi miwili.

Baadaye alipekwa katika kichumba kimoja ambako mganga huyo alilivunjilia yai na kutoa ksh 50 na kumwelezea kuwa mizimu ilihitaji pesa zaidi. ‘’ nilishtuka na nikaandamana naye hadi mjini Kenol ambapo nilitoa Ksh 124,000 na kumpa’’ Alisema.

Habari nyingine:Mtangazaji wa Citizen TV - Jeff Koinange - ajuta kuuliza maana ya 'lamba lolo'

Kaana ameeleza kuwa hadi sasa amempa mganga huyo Ksh 700,000.

Mwezi jana mganga huyo alipomgia simu kuitisha pesa zaidi, alishirikiana na polisi waliokutana naye na kumkamata kwa ulaghai.

OCPD wa Muranga Kusini, John Onditi alithibitisha kisa hicho na kueleza kuwa wameuanzisha uchunguzi ili kumfungulia mashtaka mganga huyo.

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4ZyhZdmoZqlkZZ6ornTmqKaZZ2crq%2BzwGaYpqqlmba0tMieZKSrmGKEcXyPaWdmspGgsm6uwJqbmmWplnqltcuiZKStpJq0trfAZ5%2BtpZw%3D

 Share!