- Michael Ayinde raia wa Nigeria aliwasilisha kesi mahakamani kutaka kumtaliki mkewe akidai anazaa kama sungura
- Wawili hao walikuwa wamedumu kwa ndoa kwa muda wa miaka tisa
Habari Nyingine : Pasta amshukuru mkewe kwa kumshughulikia vilivyo kitandani
Jamaa mmoja mjini Lagos Nigeria alifika mahakamani akitaka kupewa idhini ya kumtaliki mkewe akidai kuwa mwanamke huyo huzaa kama sungura.
Jamaa huyo aliyetambulika kama Michael Ayindi aliiambia mahakama hiyo kuwa mkewe anawazaa watoto wengi bila kujali hali ya uchumi na mapata ya familia yao.
Habari Nyingine : Huyu ndiye binti anayefanana na Auma Obama kama shilingi kwa ya pili, tazama picha
‘’ Mke wangu anataka kuniua na watoto. Anazaa kama sungura. Chini ya muda wa miak tisa, amezaa watoto sita. Alifutwa kazini maana anahitaji muda wa mapumziko kila anapotoka kuzaa ili kwenda kujifungua tena,'' alisema
''Baada ya kujifungua mtoto wan nne, nilimsihi atafute huduma za kupanga uzazi lakini akakataa. Ilinibidi nimpeleke hospitalini kwa nguvu ili kupata huduma hiyo lakini baadaye alirudi huko kisiri siri na kuiondoa tena,'' aliongezea.
Habari Nyingine : Maiti azungumza kabla kuzikwa, amtaja aliyemtoa kafara
Michael alieleza kuwa mkewe alienda nyumbani kwao Disemba 24, 2016 na kumpigia simu kumjuza kuwa alikuwa mja mzito.
''Kuna wakati alienda kwao nyumbani kisha akanitumia ujume kuwa alikuwa mja mzito, hakurudi hadi alipojifungua mtoto na kumpa jina mtoto huyo,'' alisema
Habari Nyingine : Obama authibitishia ulimwengu yeye ni Mjaluo na anajivunia asili yake
Wengi walimuunga mkono jamaa huyo huku mkewe akifeli kufika kortini, wengi wakidai kuwa aliogopa aibu.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibX1ygJdmoZqlkZZ6ornTmqOio5liuqyx1p5ksJldorait8BmcGaZlJa2bq3NmrGamV2grq6tjKysp5%2Blp65vtNOmow%3D%3D