-Mumewe Sofia Ben anasemekana kuwa katika uhusiano na mwanamke mwingine ambaye hushinda pamoja katika klabu moja katika Barabara ya Kiambu
-Binti huyo mrembo na ‘yellow yellow’ alitambulishwa kama Maureen Wanjiru, almaarufu Moh Shiru
-Shiru alikubali kumjua Ben na kusema zaidi ya kunywa pamoja, hakukuwa na zaidi kati yao
Mumewe Sharon Mutuku almaarufu Sofia wa kipindi cha Machachari huenda anadanganya katika uhusiano na binti mmoja mrembo sana kutoka Nairobi.
Habari Nyingine: Picha za Kabogo akijivinjari na kipusa asiyejulikana zawasisimua Wakenya
Ripoti hii ni kulingana na wadokezi wanaowajua wachumba hao. Inaonekana Ben ‘alirogwa’ na uzuri wa binti huyo, Maureen Wanjiru, almaarufu Shiru Moh, licha ya kuwa katika ndoa kwa miaka 5.
Wawili hao wana mabinti wawili warembo na mara kwa mara huonekana kupigwa picha moto moto pamoja na kuzipakia mitandaoni.
Habari Nyingine: Lavalava wa WCB ya Diamond ana kashfa nzito, amemtelekeza ‘dem’ mjamzito
Lakini ni kama mambo yamebadilika, “Ben na binti huyo mrembo wamekuwa wakibugia vileo pamoja katika klabu moja katika barabara ya Kiambu na huenda wanaendeleza uhusiano,” mdokezi mmoja alisema.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Mdokezi huyo alieleza kuwa wawili hao saa zingine hunywa na kuonekana kushikana kimapenzi hata bila kujali uwepo wa watu wengine klabuni humo baada ya kulewa.
Habari Nyingine: Picha za kupendeza za bintiye Kalonzo Musyoka
“Huwa wanakuja hapa kunywa na kufanya mambo mengine hadi usiku sana kumaanisha kuwa huenda kuna zaidi ya urafiki wa kawaida,” alisema mdokezi huyo ambaye hakutaka jina lake kutajwa.
Sofia hata hivyo alikataa kuhusishwa na suala hilo alipopigiwa simu kuulizwa.
Hata hivyo, Shiru alisema zaidi ya kuwa marafiki wa pombe, hakuna jingine ambalo hufanya pamoja.
Habari Nyingine: Je, wamfahamu babake Gavana wa Mombasa Hassan Joho?
“Ni kweli, Ben ni rafiki yangu na tunakunywa pamoja na hakuna zaidi ya hilo. Hakuna uhusiano wa kimapenzi,” alisema Shiru.
Read ENGLISH VERSION
Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News
Subscribe to watch new videosSubscribe to Tuko youtube channel to watch more interesting videos
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibYF2f5FmpK6llayybr%2FOn6CaZaeWeq6twqGYnKCRp7Zurc6nnKSZnpZ6r62Mpq6appGiuKZ5zLCgp5%2BZo7JvtNOmow%3D%3D