Kalonzo Musyoka: Nilipatana na Paulina Akiwa Kidato cha Pili "alikua maridadi"

- Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na mke wake Paulina walioana mwaka wa 1985, na wamejaaliwa watoto wanne - Kalonzo amefichua kwamba akiwa kidato cha nne, alipatana na Pauline wakati huo akiwa kidato cha pili

- Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na mke wake Paulina walioana mwaka wa 1985, na wamejaaliwa watoto wanne

- Kalonzo amefichua kwamba akiwa kidato cha nne, alipatana na Pauline wakati huo akiwa kidato cha pili

- Makamu rais huyo wa zamani alivutiwa na nywele ndefu, umbo lake Pauline na urembo, huku akijiambia kwamba siku mmoja atafunga pingu za maisha naye

Aliyekua makamu wa rais na kiongozi wa Wiper kalonzo Musyoka amewaacha watu vinywa wazi baada ya kufichua jinsi alivyo patana na bibiye Pauline Musyoka.

Habari Nyingine: Kenya Airways Yasitisha Safari za Ndege Kuelekea Uingereza

Mwanasiasa huyo alikua akizungumza katika kituo cha runinga cha maisha magic east alipodokeza kwamba alimpata Paulinea akiwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya upili ya mlango.

Wakati huo wakiwa katika kongamano la wakristo mwaka wa 1972.

Habari Nyingine: Polisi Watibua Kikao cha TangaTanga na Wanahabari Hotelini Kuhusu Mkopo wa IMF

"Alikua katibu wa chama cha wakristo katika shule yake ya mlango, alikua unapendeza umbo lake ndefu, na mtanashati nywele zake zilikua ndefu na baada ya hapo nikajua mwanamke mwema anatoka kwa mungu" alisema Alonzo

Kweli jinsi wasemavyo kwamba yaliyo fwata ni historia, wawili hao wamebaki msingi dhabiti huku Pauline akisimama kidete kulinda familia yake kutoka kwa uma.

Mwaka wa 2019, Kalonzo alifichua habari kuhusu ugonjwa wa bibiye uliopelekea Pauline kuzuru hospitali mara kwa mara tangu mwaka wa 2015.

Habari Nyingine: Matokeo ya KCPE Kutangazwa Baada ya Wiki Mbili, Waziri Magoha Asema

"Nipo katika mawazo kwa sasa, niko na bibi mgonjwa wala sigombei kiti chochote, sina kipato kinacho niita baba, watu wanakuangalia ukiwa chini na kukurushia mawe." Alisema Kalonzo

Kwenye kitabu chake, Kalonzo anasimulia jinsi alivyo taka kujua kumuoa Pauline akiwa bado na umri mdogo huku naye Pauline akionekana kutokuwa tayari kutulia kwa ndoa.

Akiwa mwanafunzi wa sheria katika chuo kikuu cha Nairobi, Kalonzo alianza mipango ya kufunga ndoa hata hivyo mchumba wake Pauline alipuuzilia mbali na kumwambia angependa kumalizia masomo yake ng'ambo.

Habari Nyingine: Magazeti Jumanne, Aprili 6: Ujanja Wakenya Wanatumia Kutoroka Kaunti za 'Lockdown'

"Nilijiambia kwamba huyu mwanamke hatilii maanani uhusiano wetu" aliandika kalonzo

Kalonzo alielekea Cyprus kufanya Stashada yake katika somo la biashara na usimamizi mjini Nicosia, wote walirejea nchini baada ya miaka saba na kufunga ndoa.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZYR6gpNmopqkn6PHsHnMrqqyp5uWeq%2B1y6KnmqyRo65uusBmp5qtnJ67onnApKCwmV2gtqWt06hknKCRYr2quMhmmKWhm6qubrnAq6CdmZSee6nAzKU%3D

 Share!