Bweni la Shule ya Upili ya St. Bridgit's, Kiminini Lateketea, Chanzo cha Moto Hakijabainika

Wanafunzi wa shule ya upili ya St. Bridgit's Girls Kiminini wanakadiria hasara baada ya moto kuteketeza bweni lao usiku wa Jumanne, Agosti 10, 2021. Moto huo unasemekana kuteketeza orofa mbili za juu za bweni hilo, hata hivyo chanzo chake bado hakijabainika kufikia sasa.

  • Bweni la shule ya Upili ya St. Bridgit's Kiminini limeteketea na mali ya thamani iliyojulikana kuharibika
  • Hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa kwenye mkasa huo kulingana na taarifa ya mwalimu mkuu Invioleta Lukorito
  • Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha moto huo

Wanafunzi wa shule ya upili ya St. Bridgit's Girls Kiminini wanakadiria hasara baada ya moto kuteketeza bweni lao usiku wa Jumanne, Agosti 10, 2021.

Moto huo unasemekana kuteketeza orofa mbili za juu za bweni hilo, hata hivyo chanzo chake bado hakijabainika kufikia sasa.

Naibu kamishna wa Kiminini Henry Metto ameambia vyombo vya habari kwamba uchunguzi umeanzisha kubaini chanzo cha moto huo.

Metto alisema anashukuru Mungu hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa wakati wa mkasa huo kwa sababu wote walikuwa darasani kwa masomo ya jioni.

" Wanafunzi wote wako salama, uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha moto huo, ningependa kuwahakikishia wazazi kwamba wanafunzi wote wako salama na wasiwe na wasiwasi," Metto alisema.

Wazima moto kutoka idara ya Trans Nzoia walifika shuleni humo pindi walipoarifiwa kuhusu mkasa huo na waliweza kuudhibiti moto huo kabla ya saa sita usiku.

Pia soma

Wanafunzi 4 Wafukuzwa Shuleni Baada ya Kumuibia Mwalimu Mkuu Mbuzi

"Maafisa wa polisi kutoka eneo hilo pamoja na washikadau walishirikiana kuuzima moto huo ingawa hatujabaini kiwango cha mali iliyoteketea," Metto aliongezea.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Inviololeta Lukorito alisema uchunguzi na makadirio yatafanywa kubaini chanzo cha moto huo na mali iliyoteketea.

" Baadhi ya wanafunzi wamepoteza bidhaa zao, tunashukuru kwamba wote wako salama, hakuna aliyejeruhiwa kwenye mkasa huo, tutafanya makadirio kuhusiana na mkasa huu," Lukorito alisema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Elimu kaunti ya Trans Nzoia Dkt. Salome Maina aliwaambia wanafunzi wasiwe na hofu ila wazingatie masoma akiwahakikishia kwamba suala hilo litashughulikiwa ipasavyo.

" Tuko nanyi pamoja kama idara ya elimu kaunti ya Trans Nzoia. Sahau yaliotendeka na mzingatie masomo ili muendelee kuinua shule yenu juu kimasomo kama ilivyo kawaida yenu," Maina aliongezea..

Mashirirka ya usalama yakishirikiana na kampuni ya umeme Kenya Power yanatarajia kufika shuleni humo kufanya makadirio ya mali iliyoteketea.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Pia soma

GOAT: Mwanariadha Eliud Kipchoge Awika Kule Tokyo Olympics

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ39xfJRmmbCdnp56ra2MrJ%2BupJVixqJ51KmgpaFdrq5uv9NmmauhlJy2tb%2BMpKCmoZ6eu6p5y5qrnqOVqbKiecKhmKeyn2Kwqa2Mpqatp12drqy1yZqZmqGenriiesetpKU%3D

 Share!