Watu 2 Wafariki Dunia, Wengine 8 Hawajulikani Waliko Baada ya Mashua Kuzama Ziwa Victoria

Watu wawili wameaga dunia na wengine 8 hawajulikani waliko baada ya mashua waliokuwa wakisafiria kuzama majini katika Ziwa Victoria karibu na ufuko wa Pier ulioko mjini Homa Bay. Waathiriwa walikuwa wanasafiri kwenda ufuko wa Ndhiru kata ndogo ya kaunti ya Mbita siku ya Jumanne wakati kisa hicho kilitokea, watu sita wameokolewa kufika sasa na wanapokea

  • Watu wawili wamepoteza maisha yao baada ya mashua waliokuwa wakisafiria kuzama kwenye Ziwa Victoria eneo la Homa Bay
  • Imeripotiwa kuwa watu wengine 8 hawajulikani waliko, shughuli za kuwatafuta zinaendelea kwa sasa
  • Aidha, watu sita wameokolewa kutokana na ajali hiyo iliyotokea Jumanne, Septemba 21 majira ya jioni
  • Miili ya wawili hao iliyoopolewa na wavuvi ilikuwa ya mwanamke na mtoto wa mwaka mmoja na nusu na imehifadhiwa katika mochari ya hospitali ya rufaa ya Homa Bay

Watu wawili wameaga dunia na wengine 8 hawajulikani waliko baada ya mashua waliokuwa wakisafiria kuzama majini katika Ziwa Victoria karibu na ufuko wa Pier ulioko mjini Homa Bay.

Waathiriwa walikuwa wanasafiri kwenda ufuko wa Ndhiru kata ndogo ya kaunti ya Mbita siku ya Jumanne wakati kisa hicho kilitokea, watu sita wameokolewa kufika sasa na wanapokea matibabu.

Mashua hiyo inasemekana kuzama takriban mita 400 kutoka ufukoni, imeripotiwa kuwa ilikuwa imebeba watu kupita kiasi na mizigo mingi ikiwemo simiti, mbao , mabati na vyakula.

Pia soma

Watu 3 Wapigwa Risasi Katika Sherehe ya 'Baby Shower' Kufuatia Mzozo Kuhusu Zawadi

Kulingana na chifu wa Homa Bay mjini Joshua Ochogo, miili ya wawili hao iliyoopolewa na wavuvi ilikuwa ya mwanamke na mtoto wa mwaka mmoja na nusu.

Akidhibitisha kisa hicho, Ochogo alisema watu sita waliokolewa walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Homa Bay kwa matibabu huku miili ya wawili hao imehifadhiwa katika mochari ya hospitali hiyo.

Aidha, shughuli za kuwasaka watu nane ambao hawajulikani waliko bado zinaendelea, wavuvi na wasamaria wema wanaoendesha shughuli hiyo wamesema nane hao wanahofiwa kufariki dunia.

Chifu wa eneo hilo alisema mashua hiyo ilikuwa imebeba abiria na mizigo kupita kiwango ambacho inafaa kubeba na ndio chanzo cha ajali hiyo.

Wakazi eneo hilo wameonywa dhidi ya kuabiri mashua ambayo imejaza hasa mizigo na wamehimizwa kuvalia vifaa vya kinga kila mara.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ4N6hJBmrpqspWJ%2FbsPAn5iroZueeqXBzaKYZq%2BVo7SqusRmb2agkayuq8HLoqKapplixKK4yKSmZpqRlrGiediaZKaZo53ConnKrrGapZFix6rDwGatopukpL%2BqrY2hq6ak

 Share!