Kauli ya Mhariri: Makala haya ni kutoka kwa Alex Opati Mulinge ambaye ni mdadavuaji wa masuala ya siasa na Biashara. Kumbuka kauli iliyotolewa hapa ni ya mwandishi binafsi na wala sio msimamo wa TUKO.co.ke.
Wanasiasa kadhaa kutoka Kisii wametangaza nia ya kumrithi Gavana James Ongwae katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Ongwae anatumikia muhula wake wa pili na wa mwisho.
Wale ambao wameonyesha kuvutiwa na na kiti hicho ni pamoja na Naibu Gavana Joash Maangi, wabunge Richard Onyonka (Kitutu Chache Kusini), Ezekiel Machogu (Nyaribari Masaba), Simba Arati (Dagoretti Kaskazini) na Seneta wa Kisii Sam Ongeri.
Wengine ni katibu wa Uangalizi wa Utawala wa Gusii Racheal Otundo na wabunge wa zamani wa Mugirango Kusini Omingo Magara na Manson Oyongo.
Maangi alisema ana kile kinachohitajika kushinda wadhifa wa juu katika kaunti. Alisema amefanya tathmini yake eneo hilo na ana hakika atakamata wadhifa huo 2022.
“Nimeweka mikakati ya kuchukua kutoka kwa Gavana James Ongwae. Ninataka kukuhakikishia kuwa nitawashusha wawaniaji wengine wote,” naibu gavana alizungumza kwenye hafla moja Julai, 2021.
Magazeti Ijumaa: UDA Yaendelea Kupata Umaarufu Mt Kenya
Kwa upande mwingine kuna Onyonka ambaye kulingana na yeye, anafaa zaidi kurithi kiti cha gavana kutokana na uzoefu wake katika siasa hasa baada ya kutumikia wadhifa wa waziri msaidizi na mbunge. Anasema ana ajenda ya maendeleo kwa kaunti hiyo.
“Nina uadilifu na uzoefu. Watu wangu wananiamini, ndiyo sababu walinichagua kuwa mbunge kwa vipindi vitatu mfululizo," Onyonka alisema.
Naibu kiongozi wa chama cha Ford Kenya na mtoto wa waziri wa zamani wa Zachary Onyonka alisema anataka kuchukua wadhifa mkubwa wa kisiasa ili kuwahudumia watu wa kaunti ya Kisii.
Mbunge huyo, hata hivyo, alisema wagombeaji wanapaswa kukumbatia demokrasia ya mazungumzo na mapatano katika kugawana viti vya juu vya kaunti hiyo.
"Wadau watakubaliana juu ya uchaguzi na uteuzi wa viongozi," alisema kwenye haffa ya awali Kisii.
Mbunge huyo ndiye mgombea pekee kutoka ukoo wa Bogetutu ambaye ametangaza nia ya kukigombea kiti hicho. Gavana Ongwae pia ni wa ukoo huo.
Kulingana na Onyonka hakuna chochote kibaya kwa mtu kutoka ukoo fulani au jamii kuchukua nafasi ya mtangulizi kutoka jamii au ukoo.
Magazeti Alhamisi: Kikosi Kinachopanga Kadi za Kisiasa za Ruto
Alitoa mfano wa Rais Uhuru Kenyatta, ambaye alichukua nafasi kutoka kwa Rais mstaafu Mwai Kibaki. Wawili hao wanatoka katika jamii moja.
Onyonka zaidi alisema Naibu Rais William Ruto, ambaye anatoka Bonde la Ufa, anatafuta kuingia Ikulu, licha ya ukweli kwamba Rais wa zamani hayati Daniel Moi, ambaye alitokea eneo hilo, alitawala Kenya kwa miaka 24.
"Wakenya huchagua viongozi kulingana na sera zao na ajenda ya maendeleo na sio koo au jamii," mbunge huyo alisema.
Kwa mujibu wa Benard Onwong'a, mtaalam wa usimamizi wa kimkakati, kuna uwezekano kwa ukoo wa Bogetutu kuridhia wadhifa wa naibu gavana kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Alisema wagombeaji kutoka kwa koo zingine huenda wakajiunga ili kuhakikisha wanapata gavana ambaye hatoki katika ukoo wa Bogetutu.
"Familia zingine ziliunga mkono Ongwae, na wanatarajia viongozi wa Bogetutu na wapiga kura kuunga mkono mgombeaji kutoka kwa koo zingine katika kaunti," Onwong'a alisema.
Aliendelea kusema kuwa: "Itakuwa ngumu kwa gavana mwingine kutoka kwa ukoo wa Bogetutu, lakini wanaweza kujadili kuhusu nafasi ya naibu gavana."
Kirinyaga: Gavana Anne Waiguru Atangaza Kujiunga na chama cha UDA
Alisema kuwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2013, ODM iligawana viti kulingana na koo.
Onwong'a alisema Gavana Ongwae atakuwa na usemi mkubwa katika uchaguzi wa ugavana wa mwaka ujao, lakini pia ana jukumu kubwa juu ya nani atamuunga mkono ikiwa viongozi kadhaa wa ODM watagombea kiti hicho.
Mapema mwezi wa Julai mwaka huu, Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga aliwakaribisha viongozi kadhaa wa eneo la Gusii kwa kile wataalam walisema kililenga kuimarisha uungwaji mkono wake Nyanza. Viongozi hao ni pamoja na Ongwae, Obure, Ong’era, Ongeri, Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’i, mweka hazina wa ODM Timothy Bosire na Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed.
Ingawa wafuasi wa Mwakilishi Kike wa Kisii Janet Ong’era na Katibu Tawala wa Barabara na Miundombinu Chris Obure wanasema wawili hao wako kwenye kinyang'anyiro cha ugavana, wawili hao binafsi bado hawajatangaza nia ya kugombea.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690
Utakuwa Unashusha Hadhi yako Iwapo Utawania Ugavana, Oparanya Amwambia Orengo
Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ4RzhJVmoqKmqZa7qK3NsqCrp11nfXN%2BjKaYo6GelnqurcqumbCZXa6uq7XTqKKespFiuLa6xpqloJmenq5uusCfmKyhXa6ubrvNoK6anV2grra606JkspldoLa0tchnn62lnA%3D%3D